Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ametwaa tuzo nyingine katika kipindi cha siku tatu zilizopita baada ya kutajwa kuwa mchezaji bora wa muda wote kwenye historia ya soka la Ureno.
Ronaldo ametwaa tuzo hiyo katika hafla maalumu iliyoandaliwa kwenye Gala Quinas De Ouro iliyofanyika huko Ureno ikiwa imeandaliwa kutoa tuzo za heshima kwa wanasoka mbalimbali wa Ureno ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 ya Shirikisho la Soka la Ureno.
Tuzo hiyo imeenda kwa Ronaldo ambaye amepigiwa kura nyingi kuliko magwiji wa soka wa Ureno akiwemo Luis Figo na hayati Euesebio ambaye alifariki dunia mwaka jana baada ya kuugua maradhi ya kiharusi kwa muda mrefu.
Ronaldo ametwaa tuzo hiyo baada ya mafanikio aliyoyapata hasa akiwa na klabu ambapo ametwaa mataji karibu yote akiwa na Manchester United na Real Madrid.
Zaidi ya hapo Ronaldo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara tatu akiwa mreno pekee kutwaa tuzo hiyo mara tatu hali ambayo imechangia kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa Ureno kwa miaka yote.
Hafla ya utoaji tuzo hizo ilihudhuriwa na marais wa FIFA na UEFA, Sepp Blatter na Michel Platinni na Ronaldo hakuweza kuhudhuria tuzo hiyo na ilipokelewa kwa niaba yake na wakala wake, Jorge Mendez.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook