Ligi kuu ya England imeendelea jioni ya leo katika viwanja tofauti nchini humo.
Viongozi waliokaa kwenye kilele cha ligi Chelsea walisafiri mpaka Cardiff kwenda kucheza na Swansea City ambao wameondokewa na mchezaji wao tegemezi Wilfred Bony aliyehamia Manchester City.
Matokeo ya mchezo huo ni ushindi mnono kabisa kwa Chelsea mwaka huu, wakishinda 5-1.
Magoli ya Oscar na Diego Costa katika kipindi cha kwanza yaliipeleka Chelsea mapumziko wakiwa wanaongoza 4-0, Oscar na Costa wakifunga mara mbili mbili kila mmoja.
Kipindi cha pili dakika ya 80 Andre Schurrle alifunga goli la tano na kuhitimisha kalamu ya magoli ya Chelsea.
Huko Villa Park, Liverpool wameendelea kupata matokeo chanya baada ya kuifunga Aston Villa 2-0.
Unahitaji kupata kila story inayonifikia mtu wangu? Ni rahisi sasa, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook