Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, Samuel Eto’o Fils anakaribia kuihama klabu ya Everton ambapo kuna taarifa kuwa atajiunga na Sampdoria ya Italia ndani ya saa chache zijazo.
Eto’o alisaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Everton lakini amekuwa akisugua benchi baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza hali ambayo imeshawishi kuhama na kwenda mahali ambako atakuwa akipata nafasi ya kucheza.
Eto’o ameshindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Everton baada ya kocha Roberto Martinez kupendelea kuwatumia Romelu Lukaku na James Naismith ambao wamekuwa wakiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Jamaa alijiunga na Everton baada ya kuichezea klabu ya Chelsea kwa msimu mmoja akiwa anatokea nchini Urusi ambako alicheza Anzhi Makhachkala ya nchini humo.
Mshambuliaji huyu alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Cameroon mara baada ya michuano ya kombe la dunia iliyopigwa mwaka 2014 nchini Brazil.
Hakuna Story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter, instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook