Spika wa Bunge Anne Makinda amesema sio kazi yake kuwasimamisha wenyeviti wa Kamati za Bunge ambao wanatuhumiwa na ishu ya fedha za Escrow badala yake ni wao wenyewe kujiondoa kama njia ya kutii maazimio yaliyopitishwa na Bunge ambayo yanawataka kuwajibika.
“Azimio linasema viongozi wa Kamati hizi watawajibika kwenye Kamati zao, tusibadilishe maneno. Naona na gazeti lingine linasema hawajajiuzulu, what is that? Suala la azimio kwamba viongozi hawa watatu wa Kamati wajiuzulu”—Anne Makinda
Askari wawili wa kituo cha Ikwiriri, Mkoa wa Pwani wameuawa na majambazi ambao idadi yao haijafahamika na kupora bunduki tano, risasi 60 na mabomu mawili ya machozi jana.
“Walikuwa ni majambazi wengi, walivamia na kuanza kuwashambulia askari wetu, walifanikiwa kuwaua askari wetu wawili na kuchukua silaha… Jeshi la Polisi nchini linalaani tukio hilo ni baya”– Advera Bulimba, msemaji wa Jeshi la Polisi.
Isikilize taarifa yote hapa niliyorekodi kwenye Habari ITV, bonyeza play.
Nitakusogezea kila story inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook