Mjadala kuhusu kuwepo sheria ya kudhibiti uvutaji wa sigara hadharani uliwahi kuingia ndani ya Bunge la T’zania siku za nyuma, jitihada hizi zinafanywa na nchi za wenzetu pia.
Serikali ya Uingereza imepanga kupitisha sheria itakayowataka watengezaji wa sigara kuuza bidhaa hiyo ikiwa ndani ya pakti ambayo haina maandishi ili kusaidia kupunguza athari zinazotokana na sigara hasa kwa watoto.
“Serikali imepanga kuwasaidia kuwalinda watoto kutokana na matumizi ya sigara ambazo ni hatari kwa afya zao“:-alisema Waziri wa Afya, Jane Ellison.
Bunge la Uingereza huenda likapitisha sheria hiyo kutokana na ushawishi walioupata kutokana na mafanikio ambayo yameonekana Australia tangu mwaka 2012 ambako walianza utaratibu huo.
Waziri wa Afya wa nchi hiyo alisema Serikali imepanga mpaka kufikia mwezi March ambao Bunge linamalizika sheria hiyo iwe imepitishwa ili ianze kufanya kazi mwaka 2016.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook