Benki ya NMB juzi January 25 ilikabidhi hundi ya Tshs mil. 75 kwa ajili ya kudhamini mkutano wa mwaka wa maafisa wa Jeshi hilo yanayofanyika Dodoma, leo kuna taarifa kwamba Benki hiyo imekabidhi pikipiki 5 aina ya Honda kwa jeshi la polisi kwa ajili ya kusaidia kazi za kila siku za jeshi hilo katika hafla iliyofanyika nje ya ukumbi wa St. Gasper katika mkutano wa maafisa wa polisi unaoendelea Dodoma.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Tom Borgols alikabidhi pikipiki hizo ambazo thamani yake ni Mil. 10 kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe.
“Tunashukuru sana kwa hizi pikipiki, zitatusaidia sana kuboresha utendaji wa polisi, tutaendelea kuwa wadau wenu muhimu” — Waziri Mathias Chikawe.
Team ya NMB ipo Dodoma kwenye mkutano huo huku huduma mbalimbali za Benki hiyo zikitolewa kwenye mabanda kadhaa ya maonyesho nje ya ukumbi wa St Gasper ambapo unafanyika mkutano huo.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook