Manchester United imethibitisha kuwa itafanya jaribio la mwisho la kumsajili beki wa kimataifa wa Ujerumani Mats Hummels zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili la mwezi januari .
United imekuwa ikimsaka Mats Hummels tangu wakati wa dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi ambapo beki huyo alisisitiza kuwa angependa kuendelea kubaki na timu yake Borrusia Dortmund lakini United bado haijakata tamaa ya kumsajili .
Beki wa Borrusia Mats Hummels amekuwa akisakwa kwa udi na uvumba na Manchester United.
Hadi sasa United imejiwekea malengo ya kusajili angalau beki mmoja wa kiwango cha juu na mpaka sasa kuna orodha ya wachezaji wwwili akiwemo Mats pamoja na beki wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte .
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ambavyo viko ndani ya United klabu hii itajaribu kusajili mmoja kati ya wachezaji hawa ili kuimarisha safu yake ya ulinzi huku wakiwa kwenye vita ya kuwania nafasi ya kufuzu michunao ya ligi ya mabingwa .
Mats Hummels ataigharimu United paundi milioni 37 huku Aymeric Laporte ambaye ametazamwa kama chaguo la pili au mbadala endapo watashindwa kumsajili akiwa sokoni kwa dau la paundi milioni 30 .