Moja ya taarifa kubwa kutoka Dodoma wiki iliyopita ilikuwa ni suala la Benki ya NMB kutoa kiasi cha shilingi milioni 75 kwa ajili ya maandalizi na shughuli za mkutano wa Maafisa wa Polisi pamoja na kutoa pikipiki 5 zenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kurahisisha kazi za operation za polisi za kila siku.
Mbali na udhamini huo wa Benki ya NMB, Maafisa wa Polisi waliokuwa katika kikao hicho kilichofanywa kwa wiki moja walionekana kufurahishwa na huduma zilizotolewa katika mabanda ya huduma za kibenki yaliyowekwa katika viwanja vya St. Gaspar ambapo huduma mbalimbali za Benki hiyo zilikuwa zikitolewa.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook