Mashabiki wa soka Misri huenda safari hii wakasahau kwa muda ligi kuu ya nchini kwao baada ya Serikali kutangaza kuisimamisha ligi hiyo kwa muda usiojulikana baada ya kuzuka vurugu zilizotokea jana na kusababisha watu zaidi ya 20 kufariki.
Wengi wa waliofariki ni mashabiki wa timu ya Zamalek ambao walifariki kutokana na msongamano mkubwa wa watu waliokuwa wakijaru kuingia kwa nguvu uwanjani ambapo Polisi waliwafyatua mabomu ya machozi wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI.
Taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa Mashabiki wa Zamalek walikuwa wanataka kuingia uwanjani kwa nguvu bila tiketi, Polisi walijikuta wakitumia nguvu ya ziada kuwazuia ili wasifanye uharibifu uwanjani.
Tukio hili limetokea ikiwa ni miaka mitatu tangu itokee ishu kama hiyo ambapo wapenzi wa soka zaidi ya 70 walifariki wakati vurugu zilizotokea katika uwanja wa ndege wa Port Said.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook