Bado kuna utata kuhusu kinaachoendelea juu ya afya ya Bobbi Kristina, mtoto wa pekee wa Marehemu Whitney Houston, mengi yanaendelea kuzungumzwa kuhusu hali yake huku wengine wakisema kuwa leo ni siku ambayo familia hiyo imeruhusu madaktari kumtoa mashine ya kupumulia ambayo aliwekewa toka siku ambayo alifikishwa hospitali baada ya kukutwa akiwa ameanguka ndani ya bafu, Georgia Marekani.
Baada ya yote kusikika familia ya Bobbi imeamua kutumia kampuni ya wanasheria wao kutoa maelezo rasmi kuhusu kila ambacho kimesikika juu ya hali ya mtoto huyo, taarifa hiyo imekanusha uvumi wote uliowahi kusikika ikiwemo ishu ya kumtoa mipira ya kupumulia siku ya leo ambapo ni siku ambayo mama yake alifariki.
Katika taarifa hiyo ya Wanasheria wa familia hiyo wamesema wanaangalia namna ya kuwachukulia hatu wote waliotoa taarifa za uongo ikiwemo waliosema walizungumza na wahusika wa familia hiyo kitu ambacho sio kweli.
TMZ, The National Enquirer, The Atlanta Journal Constitution na the Daily Mail ni sehemu ya vyombo vya habari ambavyo vimelaumiwa kwa kuandika taarifa za uongo.
Bado hakuna taarifa rasmi ambayo familia hiyo imetoa kuhusu hali ya mtoto huyo, leo inatimia miaka mitatu tangu afariki Whitney Houston ambaye alikutwa pia ameanguka bafuni.
Hautopitwa na story yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook