Nimekurekodia na kukuwekea kile kilichosomwa Magazetini leo February 13, kwenye Show ya Power Breakfast Clouds FM, unaweza kusikiliza hapa.
Kwenye zile zilizosikika kwenye uchambuzi wa Magazeti leo iko taarifa kuhusu NEC kusogeza mbele zoezi la uandikishwaji katika daftari la kudumu la wapigakura, biashara ya mende kushamiri China, rubani wa ATC kizimbani kwa kuhujumu uchumi, wanandoa waliokuwa wakisakwa kwa kujihusisha na ujambazi watiwa mbaroni Mpanda, Jeshi la Polisi lapiga marufuku maandamano ya Jumuiya ya vijana wa CUF na ishu ya mauaji mteja wa gari, mtuhumiwa alisakafia uwanja wote ili kuficha ushahidi.
Katika uchambuzi wa Magazeti kulikuwa na mazungumzo na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa ambao wamezungumzia kuhusu kusogezwa mbele kwa zoezi la uandikishwaji katika daftari la kudumu la wapigakura, pia kulikuwa na mazungumzo kutoka kwa Meneja wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) akizungumzia siku ya Radio Duniani ambayo ni leo February 13.
104.1 Clouds FM inasikika ukiwa Bukoba.
Bonyeza play hapa chini ili kusikiliza stori zote…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook