Ishu ya Panya Road ilikuwa moja ya taarifa zilizoshtua na kuathiri wengi ndani ya Dar es Salaam, ni zaidi ya mwezi mmoja tangu kumeibuka mengi kuhusu vijana hao ambao wametajwa kufanya vurugu na uhalifu.
Hii ilisikika kwenye AMPLIFAYA jana February 12, kijana mmoja Said maeneo ya Yombo amefariki, kisa kilianza alipoingia kwenye mkumbo wa vurugu, watu wakawaita Panya Rod, akapigwa na kuuawa.
Shuhuda mmoja alisimulia tukio lote lilivyokuwa; “Ninavyosikia mwisho wa lami kulikuwa na shughuli, wakawa wameenda hapo. Kuna kundi la vijana kutoka Sigara au Buza wakawa wamekuja katika shughuli, mmoja alikuwa na panga akampiga Said ambaye ni marehemu, akamnyang’anya simu yake.. wakawa wamefanya fujo pale…”
Wale vijana wa huku Machimbo wakawa wamerudi, kukatokea shughuli nyingine, kijana mwingine akawa amechanjwa viwembe na wale wa kundi la kule. Hawa wa huku wakasema mbona wanatuonea sana, kila tukienda wanatufanyia fujo? Inabidi na sisi tukawafanyie fujo..“
Kesho yake Said hakwenda kazini akasema anaumwa, akaaga kuwa anaenda kununua dawa.. wakakutana na wenzie wakawafuata kule wakawafanyia fujo wakawapiga.. wakapiga simu Polisi, wengine wakapiga kelele ‘Jamani Panya Road’.. wanakijiji wakatoka, mwenye fimbo.. rungu.. wakawa wanawakimbiza wale wa Machimbo. Said hakukimbia akasema mimi sijaiba ila nimeibiwa.. Mmoja akarusha panga likampata Said akawa amedondoka chini wanakijiji wakamvamia wakampiga“
Polisi wakamchukua wakamuweka ndani ya gari Said akawa amezimia, baadaye Said kuzinduka akamuona mvulana anayefahamiana naye akamwambia naomba kawaambie nyumbani mimi naondoka nimekamatwa.. wakati anaongea wakampiga rungu la kichwa akawa amekata kauli, hakuongea tena.. ni vilio tu vilitawala pale mtaani“
Shuhuda huyo alimzungumzia Said kuwa ni kijana ambaye hakuwa na tabia yoyote ya wizi; “Ni kijana mdogo sana, hana tabia yoyote ile mbaya Said.. msiba umewauma wengi sana..“
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook