Wengi wetu tunashukuru mabadiliko ya duniani, Sayansi na Teknolojia imefanya vitu vingi vimekuwa rahisi sana, lakini kuna upande ambao hii haiko sawa kwao, biashara zao zimaingia kwenye wakati mgumu, sababu ni hayahaya mabadiliko ambayo wengine wanafurahia!
Matumizi ya mitandao ya kijamii imatajwa kuchangia kuua soko la kadi pamoja na maua yaliyozoeleka kununuliwa msimu huu wa Valentines Day.
Baadhi ya wauza maduka ya kadi na maua katika maeneo mablimbali wamelalamikia kuporomoka kwa soko la bidhaa hizo tofauti na siku za nyuma ambapo zilikuwa zikiuzika kwa kiwango kikubwa.
Muuza duka mmoja amesema kwa mwaka huu hali ni mbaya zaidi kwani hakuna biashara ya kadi wala maua kama ilivyokuwa siku za nyuma hali, watu wanatumiana kadi na maua kupitia mitandao ya kijamii kama Whatsapp, Instagram, Facebook na Twitter.
Wauzaji hao wamesema kuwa walitegemea msimu huu biashara ingechangamka na wangeuza sana lakini imekuwa tofauti, ni watu wachache wanaojitokeza.
Chanzo cha Story hii: Gazeti la MTANZANIA, 14 Feb. 2014.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook