Kama ilivyo kawaida kukuwekea Magazeti yakisomwa hewani kwenye Redio, leo February 17, nimekuwekea kile kilichosomwa Magazetini kwenye show ya Power Breakfast ya Clouds FM, yakisomwa na kuchambuliwa na Paul James.
Miongoni mwa taarifa hizo ipo Habari inayohusu Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amemsimamisha kazi kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya bandari kwa tuhuma za utendaji mbovu, mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aporwa akiwa mikononi mwa mama yake Geita, Jeshi la Polisi linachunguza vijana wa JKT ambao walitishia kuandamana, wanafunzi wazua tafrani baada ya kufunga barabara kupinga wenzao kugongwa, mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe amewataka wamiliki wa malori ya mafuta kutafuta biashara nyingine kabla Serikali haijaachana na usafiri huo, SUMATRA imesema haijapata malalamiko yanayoitaka ishushe nauli, mwandishi wa habari apumzishwa mahabusu baada ya simu yake kuita akiwa Mahakamani, Rais Jakaya Kikwete aongoza mazishi ya aliyekuwa Chifu wa Wahehe huko Iringa, Mto Ruaha uko hatarini kutoweka endapo hatua za kuunusuru hazitachukuliwa, mfanyakazi wa chumba cha maiti Ghana akiri kupenda kufanya ngono na maiti, Kaimu kamanda wa Polisi Tanga amesema wahalifu waliovamia mkoani humo ni kikundi cha kihuni.
Katika uchambuzi huo kulikuwa na mahojiano na wahariri mbalimbali wa vyombo vya Habari nchini ambao wamelalamika Jeshi la Polisi kutotoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya matukio yanayoendelea Tanga na kuvifanya vyombo vya habari kukosa taarifa sahihi juu ya kile kinachoendelea, jambo ambalo linachangia kuwepo kwa taarifa zisizo sahihi.
104.1 Clouds FM inasikika ukiwa Bukoba.
Bonyeza play hapa chini ili kusikiliza stori zote…
https://soundcloud.com/millard_ayotv/magazeti-feb-17-clouds-fm-mp3
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook