Waziri wa elimu Liberia, Etmonia Tarpeh ametangaza kufunguliwa kwa Shule zilizokuwa zimefungwa kwa zaidi ya miezi sita nchini humo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Ufunguzi huo ulipangwa kufanyika February 2, lakini ulisogezwa mbele ili kupata nafasi ya kusambaza vifaa vya kutosha kwa ajili ya kufanyia usafi wa mazingira na vifaa vingine kwa shule za Serikali na binafsi.
Idadi ya wanafunzi walioripoti mashuleni siku ya jana February 16 imepungua, ili kuhakikisha usalama wa watoto hao michezo imepigwa marufuku ili kuepuka kugusana, pia vimechapishwa vipeperushi vya usalama vinavyowaonesha watoto hao jinsi ya kujilinda na maambukizi.
Shirika la Afya duniani (WHO) limesema idadi ya watu waliofariki kwa Ebola Liberia ni 3,800 tangu ulipotiwe kulipuka December 2013.
Unataka niwe nakusogezea kila kinachonifikia? Ungana na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram kwa kubonyeza hapa ili niwe nakutumia kila kitu moja kwa moja >>>Facebook Twitter Instagram