Kuna neno la Kiswahili watu wengi huwa wanalitumia, “usimdharau mtu usiyemjua”, kutokana na shughuli za kila siku tunakutana wengi sana tusiofahamiana nao barabarani.
Nchi za wenzetu zile treni za umeme zinazoenda kasi ni usafiri muhimu sana, watu wengi wanazitumia kama ambavyo sisi tunatumia daladala hivi, sasa jamaa mmoja ambaye ni kama aliianza siku vibaya aliingia kwenye treni London, mtu mmoja akawa amesimama mbele yake kama kamzuia hivi, jamaa hakupenda hiyo, akamsukuma halafu akamtukana.. safari yao ikaendelea.
Mchana jamaa huyo alikuwa na Interview ya kazi, ishu ikawa kwenye jopo la wanaomhoji mmoja wao alikuwa yule jamaa ambaye alimktukana asubuhi kwenye treni, Matt Buckland ambaye ndie aliyetukanwa anasema moja ya swali ambalo alimuuliza ilikuwa hili; “nilimuuliza kama alisafiri poa kwenye treni asubuhi ya leo.. Tulicheka kwa pamoja halafu nikamuomba radhi”
Buckland aliandika kwenye ukurasa wake Twitter kuhusu ishu hiyo, hii ni moja ya Tweets zilizopata Retweets nyingi pamoja na favourites pia.
Jamaa ambaye alikutwa na noma hiyo jina lake halikufahamika, Buckland amesema jamaa huyo alikosa nafasi hiyo ya kazi sio kwa kuwa alimtukana ila kwa sababu alikosa vigezo vilivyotakiwa.
Karma – the guy who pushed past me on the tube and then suggested I go F myself just arrived for his interview…with me…
— Matt Buckland (@ElSatanico) February 16, 2015
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook