Nimekuwekea hapa Magazeti yakisomwa hewani kwenye Redio leo February 24, kwenye show ya Power Breakfast ya Clouds FM, unaweza kusikiliza.
Kwenye Headlines za Magazetini stori ni zoezi la uandikishwaji daftari la wapigakura kuanza na changamoto, vigogo 99 wa fedha za Uswisi kujulikana hivi karibuni, anayetuhumiwa kumuua rafiki yake na kuzika maiti kupandishwa kizimbani, Manispaa ya Kinondoni imesema ilipokuwa kituo cha Mwenge kwa sasa ni hifadhi ya barabara.
Kingine ni ishu ya Baraza la maadili kuwahoji watumishi wa Serikali walionufaika na fedha za Escrow na Mahakama Kuu kufuta kesi nne za dawa za kulevya kwa sababu zilisajiliwa kwa makosa.
Kuna sehemu ya mahojiano na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Julius Malaba ambaye amesema zoezi la uboreshaji wa daftari la kupiga kura limeanza katika Mkoa wa Njombe na linaendelea vizuri ingawa kumekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya baadhi ya watu wenye vidole sugu kushindwa kuonekana vizuri kwenye mashine za BVR, tatizo ambalo linatokana na baadhi ya watu kufanya kazi ngumu kwa kutumia mikono.
100.5 Clouds FM inasikika ukiwa Nachingwea.
Bonyeza play hapa chini ili kusikiliza stori zote…
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook