Wanafunzi wawili Thailand wamejikuta wakiingia kwenye mikono ya Sheria kutokana tu na igizo ambalo walitunga kwa ajili ya maazimisho ya miaka 40 ya wanafunzi wa chuo hicho kupigwa na wanajeshi wa Thailand mwaka 1973 walipoandamana kudai demokrasia.
Maazimisho yao hayakuwa na heri kwa wanafunzi wawili Patiwat Saraiyaem na Porntip Mankong ambao waliandaa igizo hilo la jukwaani.
Igizo lilionekaa kukejeli uongozi wa Mfalme wa nchi hiyo, kesi ikaenda Mahakamani wakahukumiwa kwenda gerezani kwa miaka miwili na nusu kila mmoja, mchezo huo wa ‘The Wolf Bridge’ ulichezwa katika jukwaa la chuo kikuu cha Thammasat, Bangkok.
Hukumu ya wanafunzi hao ilikuwa kifungo cha miaka mitano kila mmoja lakini walipunguziwa hukumu hadi miaka miwili na nusu baada ya kukiri kosa.
“Mahakama imejiridhisha kuwa ushiriki wao katika mchezo wa jukwaani umeudhalilisha utawala wa kifalme, lakini baada ya kuirahisishia mahakama kwa kukiri kosa tuliamua kuwapunguzia kifungo“; alisema Jaji wa Mahakama.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook