Hekaheka hii inatoka Kinondoni Dar, ishu ni kesi ambayo tayari imefika kituo cha Polisi Oysterbay ambapo mwenye nyumba mmoja amekuwa akichukua kodi kwa wapangaji wengi ambao wanaletwa kwa nyakati tofauti halafu anawadanganya kwamba kuna watu wanakaribia kuhama vyumba vitakuwepo kitu ambacho sio kweli.
Baada ya wapangaji hao kushtuka kwamba wanafanyiwa utapeli mmoja wao alimkamata mwenye nyumba huyo na kumpeleka Kituoni hapo, amekaa kwa zaidi ya wiki moja huku wakipewa taarifa na askari kwamba madeni ya wapangaji hao inakaribia milioni 40 na mwenye nyumba huyo hana hela kuwalipa wote wanaomdai.
Majirani wa nyumba hiyo wamesema kuwa hiyo nyumba ni ya urithi ambayo ndugu wamegawana vyumba na kupangisha lakini huyu amekuwa na tabia ya utapeli na pia ana tabia ya kuwaibia wapangaji wake ambao tayari wanaishi hapo, anawapa funguo moja moja za milango halafu nyingine anabaki nazo, wakiwa hawapo anafungua na kuwaibia.
Hekaheka iko hapa kwa ajili yako mtu wangu, bonyeza play kuisikiliza.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook