Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Mashtaka ya Bwana Andrew Chenge katika Baraza la Maadili ni hatua moja kubwa sana katika kujenga misingi imara ya #Uwajibikaji nchini
— Zitto Ruyagwa Kabwe (@zittokabwe) February 26, 2015
Moja ya mafanikio makubwa katika sakata zima la #TegetaEscrow ni kuonyesha kuwa taasisi zipo. Iwapo zingekuwa zinafanya kazi sawasawa…. — Zitto Ruyagwa Kabwe (@zittokabwe) February 26, 2015
Moja ya adhabu Chenge anaweza kupewa ni kuzuiwa kabisa kushiriki katika uongozi wa umma. Jambo lolilopaswa kufanyika miaka mingi nyuma
— Zitto Ruyagwa Kabwe (@zittokabwe) February 26, 2015
Kitendo cha mtuhumiwa wa maadili Bw. Chenge kutumia zuio feki la mahakama ktk bunge ni dalili tosha kuwa anajua uzito mkubwa wa tuhuma zake — Zitto Ruyagwa Kabwe (@zittokabwe) February 26, 2015
Natumai kuwa Leo Baraza la Maadili litaendelea na kazi yake kwani zuio lile halihusu masuala ya maadili. Kesi dhidi ya Chenge ni muhimu mno
— Zitto Ruyagwa Kabwe (@zittokabwe) February 26, 2015
Twitter ni shule mapumziko nenda Instagram
— Nick Mweusi (@nikkwapili) February 26, 2015
Asante sana kwa support yako uliyoitoa kwa namna Moja ama nyingine katika mazishi ya ndg yetu Moses. RIP Mez B.
— Noorah (@BabaStylz) February 26, 2015
@rayc1982: Najua Kuna Wajasiriamali wenzangu naona wameanza kupagawa na mauzo ya Bidhaa zangu naona majungu yameanza ila najiamini sana na nawaheshimu wateja wa Lotions zangu kwani ndio wanaosapoti biashara yangu!kitu dhuluma sijawahi fanya katika maisha yangu na mimi ni mtafutaji tangu nikiwa mdogo sana na ushamba wa pesa huwa sina kwani nimeshazichezea sana so ningependa tu kuwambia muda wa kujibishana kwenye mitandao sina kwani natumia mitandao kutangaza bidhaa zangu na kuwa karibu na mashabiki wangu.So negativity sipendi na ukileta shobo nakublock!
@officiallulumichael:Kwahyo kuna Magazeti yanaitwa VISA Na LETE MAMBO(tutambue uwepo wao kwanza)Sasa Sina uhakika kama ni masharti Ya Boss zao Au ni sheria yao kutopitisha muda bila sura Yangu kwenye magazeti yao tena Kwa story za kujitungia tu…Sitaki mnidhihirishie Kwamba bila Sura YANGU kwenye makaratasi yenu biashara haifanyiki….mtajiuliza Kwann nimekuja kuwaweka insta,mnajua sababu….mnajifanya ️ni ma bingwa wa kuchukua Habari kwenye mitandao Ya kijamii Na kuziboresha KWA uongo…Ichukueni na HII basi….!!
Kama kweli ️mna uhakika hata bila sura yangu kwenye makaratasi yenu kazi/biashara itakuwepo kama kawaida naomba mnidhihirishie hata ndani Ya miezi 3 tu….otherwise Basi niwe boss wenu mana bila mimi hamna mishahara…!
Endeleeni na madudu yenu…ila msije kukaa kwenye RIGHT ANGLE Mta Love show..!
NAJUA MTAPITA TU Cjui kama mna account humu ningewatag kbsa..! (Picha hapo Juu ni TBT yangu☝️☝️☝️haihusiani na makaratasi Ya kidaku).
BongoMovies.com
Baada ya juzi usiku Nuhu Mziwanda kupost picha hiyo kwenye ukurasa wake mtandaoni mashabiki walionyesha kutofurahishwa na kitendo hicho na wengihne kufikia hatua ya kutukana huku wengine wakidai kuwa amemdharirisha mpenzi wake huyo ambae ni mama wa watoto wawili.
“Naomba niombe radhi kwa waliochukizwa na picha niliopost usiku wa jana.Lakini naweza sema pia ile ilikuwa ni video yangu mpya ya wimbo wangu wa Zimataa.So ilikuwa ni promotion picture.Ila mwisho wa maneno yangu ni kuomba radhi kwa lililotokea.”-Mziwanda aliandika.
Bin Zubery
Taifa Stars kushiriki Kombe la COSAFA
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imethibisha kushiriki michuano ya kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini kufuatia mwaliko wa baraza la vyama vya soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano ya kombe la COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Malinzi amlilia Refa aliyefariki Dunia
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amepelekea salamu za rambirambi kwa familia ya mwamuzi mstaafu Mohamed Nyama ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya waamuzi ya TFF kilichotokea jana kwao Nachingwea – Lindi.
Marehemu Mohamed Nyama wakati wa uhai wake alikuwa mwamuzi wa daraja la kwanza ambaye pia alitambuliwa na FIFA.
Saleh Jembe
Kiungo Simon Sserunkuma amerejea kwao Uganda kutokana na mafanikio ya kifamilia.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza Sserunkuma amerudi Uganda kwa ajili ya shughuli ya arobaini ya mmoja wa wazazi wake.
Sserunkuma ameondoka wakati Simba ikijianda akupambana na Prisons, keshokutwa.
Kocha wa Simba, Goran Kopunovic ameonekana kutomuamini sana Simon na mara nyingi amekuwa akimuingiza katika kipindi cha pili.
TAMBWE, NIYONZIMA WAZUIWA UWANJA WA NDEGE BOTSWANA
Viongozi wa Yanga waliiongozana na timu mjini Gaborone, Botswana wamelazimika kufanya kazi ya ziada kuwakomboa uwanja wa ndege wachezaji watatu.
Wachezaji hao watatu ni Amissi Tambwe raia wa Burundi ambaye alifunga mabao yote mawili wakati Yanga ikiishinda BDF XI kwa mabao 2-0 jijini Dar. Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima (wote raia wa Rwanda).
Yanga imetua Gaborone kwa ajili ya kucheza mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho ikiwa ina mtaji wa bao 2-0 ilizozipata jijini Dar.
Wachezaji hao walizuiwa kutokana na kuwa na uraia tofauti na Tanzania na kwa mujibu wa sheria za Botswana walitakiwa kukatiwa visa.
Hali hiyo iliwafanya wakwame uwanjani hapo kwa takribani saa na ushee huku wengine wakilazimika kuanza msafara wa kwenda hotelini.
Baadaye suala hilo lilishughulikiwa na wachezaji hao kufanikiwa kulipiwa visa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook