Kamati Kuu ya CCM imezidi kuwaweka gizani makada sita waliomaliza adhabu ya kufungiwa kwa miezi 12 baada ya kueleza kuwa uchunguzi dhidi yao unaendelea kwa muda usiojulikana, uamuzi utakaowazuia kujitokeza rasmi kutangaza nia ya kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho tawala.
Edward Lowassa, Bernard Membe, Frederick Sumaye, William Ngeleja, Stephen Wasira na January Makamba, ambao walipewa adhabu hiyo Februari 18 mwaka jana, sasa watalazimika kusubiri hadi hapo Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM itakapomaliza uchunguzi wake, ikiwa imebaki miezi isiyopungua mitatu kabla ya wanachama kuanza harakati za kuwania nafasi mbalimbali.
Kwa kawaida, CCM huruhusu wanachama wake kuanza kuchukua fomu za kuwania urais, ubunge na udiwani kati ya mwezi Mei na Juni na kabla ya hapo huruhusiwa kutangaza nia ya kugombea nafasi wanazotaka, fursa ambayo makada hao wameikosa hadi sasa.
Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu, kuwa kwa kuzingatia kanuni za maadili ya CCM, mwanachama aliyepewa onyo kali atakaa chini ya uangalizi kwa kipindi kisichopungua miezi 12,
“Baada ya miezi hiyo kwisha, Kamati Ndogo ya Maadili inaendelea na kazi yake kuchunguza mienendo yao hao waliokuwa wamepewa adhabu katika kipindi chao cha adhabu cha miezi 12 kama wametekelezaje masharti ya adhabu,”:- Nnauye.
Alisema kazi ya kamati hiyo ndogo ni kuchunguza ili kubaini kama makada wote sita walitimiza masharti ya adhabu waliyopewa na kwamba itakapomaliza uchunguzi katika muda usiojulikana itapeleka taarifa Kamati Kuu.
“Itachukua wiki, itachukua mwezi, itachukua miezi ni kwamba itakapokamilika na Kamati Kuu kama kutakuwa na taarifa yoyote tutautaarifu umma juu ya kinachoendelea,” .
Kikao cha Kamati Kuu, ambacho huhusisha viongozi wa juu serikalini na kwenye chama hicho tawala pamoja na wanachama 14 wa kuchaguliwa kutoka Zanzibar na Bara, kilifanyika Ikulu na Nape aliongea na waandishi wa habari kwenye ofisi ya Umoja wa Vijana wa CCM iliyo Lumumba.
Kati ya waliofungiwa, Wasira, ambaye ni Waziri wa Kilimo na Ushirika, ni mjumbe wa Kamati Kuu.
MWANANCHI
Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mkurugenzi wa Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni John Komba amefariki dunia leo alipokuwa akipelekwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam baada ya kuzidiwa.
Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Hospitali ya TMJ, ofisi ya Bunge na Chama Cha Mapinduzi na kwamba kwa sasa taratibu za maziko yake zinaendelea kufanywa .
Aidha taarifa za hivi punde kutoka nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach Tangi Bovu zinaeleza kuwa maelfu ya watu kutoka katika kada mbalimbali wanaendelea kumiminika nyumbani kwa marehemu ili kutoa faraja kwa familia kwani marehemu ameacha mjane mmoja na watoto kumi na moja.
Akizungumza na tovuti hii mmoja wa madaktari aliyempokea wakati anafikishwa hospitali ya TMJ, Dk Elisha Ishan amesema Komba alifikishwa hospitalini hapo saa 10 jioni leo akiwa mahututi .
“Nilimpokea nilianza moja kwa moja kumpima shinikizo la damu na vipimo vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa ndugu yetu ameaga dunia,”- Dk Ishan
Pamoja na hayo Dk Ishan amekwepa kutaja moja kwa moja chanzo cha kifo cha mareheme, hata hivyo amesea Kapteni Komba alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na kwamba siku za karibuni alifika hospitalini hapo kwenye kiliniki yake ya shinikizo la damu.
MWANANCHI
Siku chache baada ya kutokea mauaji ya mtoto albino Yohana Bahati Wilayani Chato, Geita,hali si shwari katika kijiji cha Ihale Simiyu baada ya viongozi wa vijiji kumfukuza mtoto Fatuma Ally mwenye mwaka mmoja ambaye ni mlemavu wa ngozi pamoja na mama yake kwa madai ya kumtaka kwenda kumtafutia sehemu salama.
Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 4 pamoja na mama yake Neymar Hamis walifukuzwa kijijin hapo kwa madai mtoto huyo mwenye ulemavu hana ulinzi wowote.
Mama wa mtoto huyo alisema baadhi ya viongozi wa kijiji chake akiwemo ofisa mtendaji walimwandikia barua ya kumtaka kwenda kituo cha kulelea watoto yatima cha bikira maria kilichopo mjini.
Mama huyo alisemabaada ya kuandikiwa barua alikwenda katika kituo hicho na kumkuta mlezi wake SiSter Maria ambaye alimweleza sababu ya kumpekea mwanaye hapo
NIPASHE
Shirika la viwango nchini TBS limesema limewasilisha ripoti kwa polisi wa kimataifa ‘Interpol’ kuhusu sakata lamabati feki yaliyoagizwa nchini ili mzalishaji akamatwe na kuchukuliwa hatua.
Mabati hayo yalizuiwa bandari ya Dar es salaam Januari mwaka jana baada ya TBS kubaini hayakuwa na ubora.
Mabati hayo yaliangizwa nchini na wafanyabiashara wa kwema Trade Trust ltd kutoka China na mpaka sasa shehena hiyo ipo bandari kavu ikisubiri kuteketezwa.
Mwanasheria wa TBS Baptister Bitaho wameshawasilisha ripoti kwa Interpol ili iweze kuwasiliana na China kumkamata mzalishaji.
Alisema kiwanda hicho kilihusika kutengeneza mabati feki ambayo hayakupitishwa na cheti cha ubora.
JAMBOLEO
Maajabu makubwa yametokeo kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa tumbo kenye hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam baada ya madaktari kushuhudia wakitoa nyaya za umeme,funguo,pini,mashine ya kunyolea nywele,cheni na misumari.
Madaktari waliokuwa wakifanya upasuaji huo walijikuta kwenye wakati mgumu kutokana na kila walipokuwa wakiendelea na upasuaji huo wakitoa vitu vya ajabu kwenye mwili wa binadamu.
Upasuaji huo ulifanyika juzi jioni baadaya mgonjwa huyo kufikishwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kutokana na kusumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa taarifa za baadhi ya madaktari walisema walimpokea mgonjwa huyo akitokea hospitali ya Tumbi Kibaha.
Walisema mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo akiwa na maumivu makali yaliyomfanya alalamike muda wote.
“Baada ya madaktari kufanya upasuaji katika hali isiyokuwa ya kawaida,wakaanza kushuhudia ndani ya tumbo la mgonjwa huyo anatua vitu vya ajabu,na baadhi yake ni kama pini,misumari,mashine ya kunyolea nywele”alisema mmoja wa madaktari hao.
MAJIRA
Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Dodoma limeuagiza uongozi wa Manispaa hiyo kuhakikisha kuwa linajenga uzio wa kuzunguka sanamu ya mwalimu Nyerere katika eneo la Nyerere square kutokana na watu wanaopiga picha katika eneo hilo baadhi yao kupiga picha za nusu utupu.
Nyerere square kuna picha ya baba wa Taifa ambapo limekuwa eneo maarufu kwa watu kwenda kupiga picha na kuonekana na sanamu hiyo,lakini viwango vya nidhamu ya sanamu hiyo vimeanza kushuka.
Kutokana na hali hiyo Madiwani wa Manispaa ya Dodoma wameitaka manispaa hiyo kuhakikisha inajenga uzio katika eneo hilo ili kudhibiti hali hiyo kulingana na hadhi ya eneo husika na thamani ya sanamu hiyo.
Diwani wa kata ya Kikuyu John Risasi alisema manispaa inatakiwa kuchukua tahadhari ili kujenga heshima ya mnara huo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook