February 12 mwaka huu hapa hapa kwenye millardayo.com nilikusogezea story kuhusu watoto wawili mapacha kuzaliwa huku wakiwa wamepishana miezi miwili.
Kwa mujibu wa wataalamu walisema watoto hao walizaliwa katika mifuko tofauti ya uzazi ambayo iliruhusu mmoja kuzaliwa kabla ya mwenzake.
Leo tena kuna stori inayowahusu wasichana hawa Lucy na Maria ambao ni mapacha, ni mapacha lakini ukiwaangalia kwa muonekano wanaonekana tofauti kasiba, ukiwaangalia halafu ukawaambiwa ni mapacha unaweza usiamini kwamba wawili hao ni mapacha.
Kwa upande wa wazazi, baba yao Vince ni mzungu huku mama yao Donna ana asili ya Jamaica.
Lucy anaonekana ni mweupe kuanzia rangi ya ngozi hadi nywele, lakini Maria ni mweusi kuanzia rangi ya mwili wake mpaka nywele.
“Hakuna anayeamini sisi ni mapacha… hata tukivaa sare hawaamini, hatuonekani kabisa kama mapacha.. ilitubidi hata kwenda kuleta ushahidi wa vyeti vya kuzaliwa hospitali kuwahakikishia marafiki zetu..”.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook