Nimekurekodia na kukuwekea kile kilichosomwa Magazetini leo March 03, kwenye Show ya Power Breakfast Clouds FM, unaweza kusikiliza hapa.
Kwenye zile zilizosikika kwenye uchambuzi wa Magazeti leo iko taarifa inayosema takwimu zilizotolewa na Bank ya dunia zinaonyesha kuwa wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi wameweza kuingiza kiasi cha shilingi milioni miamoja thelathini na tano kwa mwaka 2013, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli amesema ujenzi wa daraja la Kigamboni ni lazima umalizike June mwaka huu, wimbo wa marehemu, Kapteni John Komba alioimba wakati wa kifo cha Baba wa Taifa waibua majonzi wakati wa kuaga mwili wake Dar, baada ya wasanii kuubadilisha maneno na kumuimbia, Rais Jakaya Kikwete amesema matukio ya watu kuvamia vituo vya Polisi nchini yana sura ya ujambazi na ugaidi ndani yake, jumla ya mabinti kumi na mbili wamenaswa na dawa za kulevya ndani ya siku thelathini, usiri wagubika kukamatwa kwa kiongozi wa CHADEMA huko Mwanza, wafanyakazi wawili wa Tanesco ambao ni wanandoa wamefariki katika mazingira ya kutatanisha huko Mbeya, NHC kujenga nyumba elfu mbili na miatano za kuuzwa kwa gharama nafuu mwaka huu na tani elfu kumi na tano za sukari zayeyuka bandarini na kuzua mjadala mkubwa.
Katika uchambuzi huo kulikuwa na mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesm Mramba, ambae ametolea ufafanuzi tatizo la Luku za umeme nchini, ambae amesema tatizo hilo limetokana na mfumo wa kutoa huduma hiyo kuwa na tatizo lakini wamefanikiwa kutatua tatizo hilo na wateja wameshaanza kupata huduma, lakini wanatarajia kuwa na mfumo mwingine mpya tofauti na huu unaotumika kwa sasa ili kuondokana na tatizo hilo.
Bonyeza play hapa chini ili kusikiliza stori zote…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook