Mara nyingi mtu akisumbuliwa na panya nyumbani kwake hufuga paka ili kuweza kutokomeza panya lakini kuna mwingine anawapenda na kuamua kufuga hata kama lengo lake sio hilo.
Huko Japan katika kisiwa cha Aoshima ulifanyika mpango wa kufuga paka kwa lengo la kutokomeza panya lakini baadaye paka hao wamegeuka kuwa kivutio kikubwa cha utalii katika kisiwa hicho ambacho watu wanaoishi hapo ni 22 pekee lakini kimezingirwa na paka.
Paka hao waliletwa wachache kuangamiza panya ambao walikuwa wakiharibu mitumbwi lakini kwa sasa paka wamezaliana na idadi yao kufikia zaidi ya 120.
Paka hao wanaishi kwa kula chakula mtaani na mabaki ya chakula yanayotupwa kwenye majalala, kisiwa hicho ambacho hakina maduka wala Hoteli kwa sasa kinajulikana kama ‘Cat Island’, paka wao kwa sasa wamekuwa kivutio cha utalii kwa wageni wanaotembelea.
Unaweza kutazama video kwa kubonyeza playa hapa mtu wangu.
https://www.youtube.com/watch?v=Y5kH13gZp84
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook