Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini Mark Lippert ameshambuliwa kwa kisu usoni na mkononi wake na mshambuliaji aliyekuwa akilalamikia kuhusiana na suala la kugawanywa ardhi ya Jumuiya yao wakati wa hotuba.
Balozi huyo alikimbizwa Hospitali ambako alifanyiwa upasuaji wa zaidi ya saa mbili kwenye jeraha na pia ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa, huku baadhi ya mishipa ikishindwa kufanya kazi ingawa madaktari wamesema hakuna athari yoyote itakayotokana na majeraha hayo.
Baada ya shambulio hilo maofisa wa Polisi walifanikiwa kumkamata Kim Ki-Jong akihusishwa na tukio hilo huku kukiwa na taarifa za jamaa huyo kufanya kosa kama hilo mwaka 2010 alipomshambulia Balozi wa Japan nchini Seoul.
Rais wa Marekani Barack Obama amempa pole Balozi huyo.
Msemaji wa baraza la maridhiano na ushirikiano ambaye ndiye muandaaji wa mkutano huo ameomba radhi kwa kutokuwa na ulinzi mzuri uliosababisha Balozi huyo kushambuliwa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook