Kila mtu ana njia yake ambayo ameitumia au ataitumia kumpata mpenzi wake wa maisha, kwa mtu ambaye yuko serious anaweza kutumia njia yoyote ili ampate yule anayemtaka, hii njia aliyoitumia Dean Smith, kutoka Arizona Marekani ni moja ya chache nilizowahi kuzisikia.
Dean Smith aliandaa video hiyo kwa Jennifer Kessel, ameiandaa kwa siku 365 akijieleza tu jinsi anavyompenda dada huyo.
Smith aliandaa video hiyo kama zawadi ya suprise ya siku ya kuzaliwa ya Jennifer amejirekodi akiwa anafanya kazi mbalimbali, sehemu nyingine yuko jikoni anapika, yuko barabarani anaendesha gari, sehemu nyingine yuko ofisini.. kote anaonekana ameshika bango lililoandika “Jennifer, will you marry me?’, ‘Will you be my wife?’, ‘Make me the happiest man in the world’, ‘I love you so much..”
Dean aliwatumia ndugu wa Jennifer wakiwemo wazazi wake kumfanyia surprise, walimtoa ndani ya nyumba yao taratibu kwa mabango ya maelekezo mwisho akaenda mpaka beach wakampa video hiyo aangalie, mwisho wa video kuna maandishi ‘Turn around‘, anageuka nyuma anakutana na Dean.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook