Nimekuwekea hapa Magazeti yakisomwa hewani kwenye Redio, leo March 10, kwenye show ya Power Breakfast ya Clouds FM, yakichambuliwa na Paul James unaweza kusikiliza.
Baadhi ya taarifa zilizochukua uzito wa juu kwenye Magazeti ni kigogo TCAA ajikaanga kuhusu sakata la mgao wa Escrow, ufisadi mwingine wa zaidi ya bilioni 252 umeibuliwa na CAG Prof. Musa Assad, Mkuu wa Wilaya ya K’ndoni, Paul Makonda ameanzisha dawati maalum la Polisi katika Hospitali ya Mwananyamala na Sinza na Jeshi la Polisi Kilimanjaro limebaini watoto 18 waliokuwa wamefungiwa ndani walikuwa wanaishi kwa mateso makubwa.
Baadhi ya wanazuoni, viongozi wa dini, wanasiasa na wanaharakati wamesema kuendelea kulazimisha kura ya maoni ni kuligawa taifa, viongozi wamemtembelea mtoto mlemavu wa ngozi aliyekatwa mkono aliyelazwa katika Hospitali ya rufaa ya Mbeya, Serikali imeanza mkakati wa kulifufua shirika la ndege Tanzania ATC na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Mwakyembe amesema ameanza kuchafuliwa kisiasa.
Katika uchambuzi huo kulikuwa na mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe ambaye amesema kuhusishwa kwake kwenye mchakato wa zabuni ya TRL sio jambo sahihi, kwani Waziri hahusiki na mchakato wa tenda kutokana na sheria kutompa Waziri mamlaka ya kuingilia.
Yeye alichukua hatua na kwenda TRL na kuagiza bodi ya Wakurugenzi kuwasimamisha kazi wote waliohusika na kuvunja bodi ya tenda pamoja na kupeleka suala hilo Takukuru, ambapo suala hilo liko huko kwa sasa, lakini kauli hiyo imetolewa kwa lengo la kumchafua kisiasa kutokana na kuelekea kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu.
Bonyeza play hapa chini ili kusikiliza uchambuzi wa story zote…
https://soundcloud.com/millard_ayotv/magazeti-march-10-clouds-fmmp3
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook