Ikitokea ishu ya kupeana support kwenye mambo mbalimbali, wasanii wamekuwa Mabalozi wazuri wa nchi kwenye kuunganisha nguvu na kufanya ushirikiano, mfano mzuri ilipofika final ya #BBAHotshots tuliona akina Jose Chameleone toka UG, Prezzo kutoka Kenya na wengine wengi wakitoa support kuhimiza watu kupiga kura ili Idris arudi na ushindi TZ, ushindi ambao unatuhusu pia East Africa yote.
Tatizo la mauaji ya walemavu wa ngozi nalo limegusa watu wengi hata nje ya mipaka ya Tz, moja ya story ambazo zimepewa headlines leo Kenya ni ishu ya staa wa muziki kutoka Kenya, Nonini kusema kwamba ana lengo la kuisogeza Kampeni yake ya #ColourKwaFace ndani ya mipaka ya Tanzania ili kuelimisha jamii iachane na imani za kishirikina ambazo zinatajwa kuwa chanzo cha mauaji hayo.
Kwenye kampeni hiyo pia Nonini amepanga kutoa vifaa ambayo vitawasaidia albino kujikinga na mionzi ya jua.
Kampeni hii sio mara ya kwanza Nonini kuifanya, aliwahi kuimba wimbo ambao unazungumzia ishu ya mauaji hayo pia.
Bonyeza play uicheki.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook