Mwanasheria wa Chama cha CHADEMA, Tundu Lissu leo ametangaza rasmi kumvua uanachama Mbunge wa Kigoma Kaskazini baada ya uamuzi wa Mahakama juu ya kesi iliyofunguliwa na Zitto Kabwe kuhusu kupinga uanachama wake kujadiliwa.
Baada ya uamuzi huo millardayo.com pia imeongea na Tundu Lissu kupata uhakika wa kinachosemekana na hizi ni sentensi zake>>’Tumemshinda.. kesi yake imefutiliwa mbali ameambiwa atulipe gharama na kwa vile ile kamali aliyocheza ya kupeleka kesi Mahakamani imeshindikana si mwanachama wetu tena sasa hii ni rasmi‘
‘Katiba yetu inasema ukipeleka kesi ya mambo ya Chama kwenye Mahakama unafukuzwa uanachama na kwa mujibu wa Katiba si mwanachama wetu tena… hilo haliwezi kuwa kosa letu akamuulize Jaji Mchome‘– Tundu Lissu.
Hata hivyo baada ya uamuzi huo Mwanasheria Alberto Msando ambaye ni Wakili wa Zitto Kabwe ameandika haya kwenye akaunti yake ya Instagram
Bonyeza play kumsikiliza pia Tundu Lissu akizungumza na millardayo.com
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook