Mechi za kufuzu kwa michuano hiyo kwaupande wa nchi za Afrika zinatarajiwa kuanza mwezi October mwaka huu, Zimbabwe ni moja ya nchi za Afrika ambazo hazijawahi kufuzu kucheza mechi za Kombe la Dunia.
Taarifa kutoka FIFA leo inahusu uamuzi uliotolewa kwamba Zimbabwe imepigwa marufuku kushiriki katika mechi za kufuzu kombe la dunia kwa mwaka 2018, baada ya kuwepo kwa taarifa za nchi hiyo kukataa kumlipa kocha wake wa zamani, Jose Claudinei Georgini.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la soka Duniani FIFA imesema kuwa, imechukua hatua hiyo baada ya nchi hilo kushindwa kumlipa kocha huyo na kuongezea kuwa shirikisho la soka Zimbabwe, ZIFA lilishindwa kulipa deni hilo mbali ya kwamba walipewa muda wa kutosha ili kufanya malipo hayo.
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook