Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2018/2019 imeendelea tena usiku wa October 23 2018 kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali Ulaya.
Game kati ya Man United dhidi ya Juventus ni moja kati ya game zilizokuwa na mvuto zaidi usiku huo, hasa ni kutokana na Cristiano Ronaldo kurudi Old Trafford akiwa na Juventus.
Ronaldo usiku huo alirudi katika dimba la Man United ikiwa ndio club aliyoanza nayo kupata mafanikio katika soka, hivyo wengi walitamani kuona kama Ronaldo ataifunga timu yake ya zamani.
Game ilifanikiwa kuisha kwa Man United kupoteza nyumbani kwa kufungwa goli 1-0, goli la Juventus lilifungwa na Paul Dybala dakika ya 18, matokeo hayo yanaifanya Juventus kuongoza Kundi H kwa kuwa na jumla ya point 9 wakifuatiwa na Man United waliopo nafasi ya pili kwa kuwa na point 4.