Aaron Ramsey, anatarajiwa kurejea Cardiff kwani makubaliano yamefikiwa ya kumsajili kiungo huyo kutoka OGC Nice ambapo kiungo huyo wa zamani wa Arsenal, 32, anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na klabu hiyo ya Championship siku ya leo.
Ramsey anapatikana kwa uhamisho wa bure baada ya mkataba wake Nice kumalizika mwezi uliopita, ingawa taarifa za mwisho bado hazijakubaliwa.
Alikuwa amevutia vilabu vingine lakini ana hamu ya kuhamia Wales kusini na familia yake.
Kuwasili kwa Ramsey kungewakilisha usajili mkubwa kwa Cardiff na nyongeza kubwa kwa meneja mpya Erol Bulut, ambaye amekuwa na nia ya kumrejesha mchezaji huyo katika klabu ambapo maisha yake ya soka yalianza akiwa kijana.
Akiwa ameichezea nchi yake mara 82, Ramsey alijiunga na Cardiff mwaka wa 2007 kabla ya kujiunga na Arsenal mwaka wa 2008. Alirejea kwa muda mfupi katika mji mkuu wa Wales mwaka wa 2011 alipopata nafuu baada ya kuvunjika mguu.