Mwanamuziki wa bongo Flava Abigail Chamungwana maarufu kama Abigail Chams leo Septemba 02,2024 ametembelea bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaliko wa spika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kwaajili ya kushuhudia shughuli za bunge.
Nje ya bunge @ayo tv tumempata nafasi ya kupiga nae stori kufahamu sababu za ujio wake bungeni lakini pia tumemuuliza kuhusiana na yeye kupanda jukwaa moja kwa mara ya kwanza na TID weekend iliyopita ni baada ya kutofautiana kupitia mitandao ya kijamii
Tulivyomuuliza kuhusu yeye kuyamaliza na TID na nini kinaendelea kati yao amesema “Unajua mimi sipendi stress kwahiyo yaliyotokea yalitokea ameomba msamaha na mimi ni mtu ambaye siwezi kumshika mtu moyoni au kushika kitu ‘we are fine’ na nilivyokutana nae nilimsalimia (shikamoo) ni babu yangu ambaye kwasasa ni rafiki yangu na tuliongea mengi na asliniomba msamaha” Abigail Chams