Matukio ya ugaidi ambayo yameendelea kutokea kwenye kona mbalimbali za dunia yameendelea kusumbua akili za watu kiasi kwamba Mfanyakazi mmoja wa hoteli moja ya Ohio Marekani alilazimika kupiga simu Polisi baada ya kuhisi Mwarabu huyu aliyevalia kanzu anaweza kuwa gaidi.
Muda mfupi baada ya maelezo kutolewa Polisi walivamia kwa mkwara eneo hilo na kumuweka Ahmed al-Menhali (41) chini ya ulinzi na kuanza kumpekua mpaka kumvua viatu huku mwenyewe akisisitiza sio gaidi bali ni mtalii.
Ahmed anasema alikwenda Marekani kwa ajili ya matibabu ambapo kwenye kama dakika kumi baada ya kuwekwa chini ya ulinzi akiwa amelazwa chini alisimamishwa na kupelekwa Hospitali kutokana na kupata majeraha madogo ambapo tayari alishasachiwa na hakupatikana na chochote.
Camera ya video iliyovaliwa na Polisi inaonyesha tukio hilo kuanzia mwanzo ambapo saa chache baadae baada ya kujulikana ni Msamaria na kwamba ilikua ni hofu tu ya Mfanyakazi wa Hoteli, Polisi walimuomba radhi Ahmed kwa kilichotokea, unaweza kutazama hii video hapa chini.
Hata hivyo Wizara ya mambo ya nje ya falme za kiarabu imewataka raia wake kuepuka kuvaa mavazi yao ya kitamaduni wanaposafiri kwenda nje ya nchi ili kuepusha kuuweka usalama wao kwenye hatari zaidi.
ULIIKOSA YA WATALII KUSITISHA SAFARI ZA TANZANIA KISA KODI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI