HEADLINES za ajali za mabasi TZ zimeendelea.. lakini wakati mwingine kumekuwa na uvumi wa mitandaoni, watu wanaambizana kuwa kuna ajali halafu PICHA ambazo zinatumiwa zinakuwa hazina uhalisia na tukio lenyewe.
Hizi zimeenea sana mitandaoni leo, nimeifuatilia na kupata undani wa taarifa yenyewe.. ni ajali iliyotokea Nzega, Tabora. RPC wa Tabora, Suzan Kaganda amethibitisha kutokea ajali hiyo, mtu mmoja amefariki na wengine 20 wamejeruhiwa baada ya basi hilo la Air Jordan kupinduka.
#BreakingNEWS: Mtu mmoja amefariki, wengine 20 wamejeruhiwa kwenye ajali ya basi la Air Jordan iliyotokea Nzega, TABORA. #RIP
— millardayo.com (@millardayo) April 15, 2015
Kingine kilichonifikia ni kuhusu ajali iliyotokea jana ambapo radi ilisababisha vifo vya watu nane Kigoma, kati yao walikuwepo wanafunzi sita wa Shule ya Msingi, mwalimu mmoja na mtu mwingine mmoja.. mazishi ya wote waliofariki yanafanyika leo.
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook