Ishu ya ajali za barabarani imechukua nafasi kubwa sana kwenye stori za kwenye vyombo vya habari TZ.. kwanza ni suala la ajali hizo kuongozana sana.. kingine ni ishu ya idadi kuwa ya vifo ambavyo vimetokana na ajali hizo.
Leo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohammed MPINGA yuko kwenye headlines; “Watu waliofariki kutokana na ajali hizi toka hiyo tarehe 11 mwezii wa tatu hadi hilo tukio la tarehe 14 takribani mwezi mmoja tu wamefariki watu 103 na kujeruhi watu 38.. katika hao watu 103 wengi ni abiria.. sababu kubwa ya ajali hizi ni makosa ya kibinadamu ambayo kwa kiasi kikubwa ni uzembe wa dereva.“
“Mweni January zimetokea ajali 823, February 641, March ni 32.. ukiangalia idadi ya watu waliokufa kwa mwezi March ni kubwa ukilinganisha na idadi ya ajali zilizotokea.“– Kamanda Mpinga.
Tumepoteza ndugu, jamaa, marafiki na watu wetu wengi kwenye hizi ajali.. #RIP kwa wote.
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook