Siku chache zimepita toka taarifa zitufikie kuhusu ajali ya basi la abiria lililotumbukia mtoni eneo la Iyovi ambalo lina kona kali sana mkoa wa Iringa, taarifa nyingine ya huzuni inatufikia kutoka mkoa wa Njombe leo January 04 2016.
Ni taarifa ya ajali ya basi la abiria ambalo limegonga lori la mizigo kwa nyuma na kusababisha vifo vya watu wawili pamoja na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.
#MillardAyoUPDATES: Watu wawili wamefariki, wengine 21 wajeruhiwa ktk ajali ya basi la LUWINZO lililogongana na lori la mizigo Njombe. #RIP
— millard ayo (@millardayo) January 4, 2016
Wapumzike kwa amani wote waliofariki, na majeruhi wapate ahueni mapema.
Hizi ni picha nne kutoka eneo la ajali nilizozipata Michuzi Blog
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE