Hizi smartphone zimerahisisha vitu vingi, lakini usidhani hiyo simu ndio haiwezi kukuletea majanga!!
Jamaa mmoja Paul Pelton alijikuta akiingia kwenye mikono ya Sheria kirahisi kabisa yani huenda hata yeye mwenyewe hakujua kwamba ataishia hapa.. alikuwa anapita kwenye barabara ambayo iko umbali wa kama Kilometa 60 hivi toka Jimbo la Cleveland Marekani, akakuta kuna watu wawili waliopata ajali, alichokifanya ni kutoa simu yake alafu akarekodi kipande cha video bila kufanya kitu kingine chochote.
Kulikuwepo watu wengine walioikuta ajali hiyo, wakawachukua majeruhi na kuwakimbiza Hospitali lakini kwa bahati mbaya mmoja wa vijana hao, Cameron Friend alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata.
Baada ya Pelton kuisambaza video jamaa walimsaka na akapatikana, kesi inaendelea Mahakamani na kama akikutwa na hatia hukumu yake itakuwa kukaa jela kwa siku 30 na kulipa faini ya Dola Mil. 250 ambazo ni zaidi ya Tshs 530,000/=
Kosa ambalo limemfikisha kwenye mikono ya Sheria ni ishu ya kuingia kwenye gari ya watu waliopata ajali na kuwarekodi video, mbaya zaidi ni kwamba hakutoa msaada wowote kwa majeruhi wa ajali hiyo.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.