Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Gabriel Makalla amekemea uwepo wa makundi baina ya wanachama wa chama hicho huku akisema kuwa suala hilo ni moja ya mambo yanayosababisha kupungua kwa kura za Chama cha Mapinduzi.
Akiongea jijini Dar es salaam katika ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Amos Makalla amesema kuwa “Makundi, hila na fitina ndizo zinazosababisha kupungua kwa kura za Chama cha Mapinduzi, wewe umechaguliwa kuwa kiongozi miaka mitano bado unasaka maadui zako kwahiyo niseme ukishachaguliwa vunja makundi fanya kazi na watu wote”.
Aidha Makalla amewasisitiza wanachama wote wa Ccm kuwa suala la umoja na mshikamano ndio silaha pekee ya kukijenga chama hicho na si vinginevyo.