Leo Septermber 7, 2020 Mzee mmoja mwenye umri miaka 80 katika Kijiji cha Parcoul-Chenaud huko Dordogne Kusini mwa Ufaransa ametekeza sehemu ya nyumba yake akijaribu kufukuza nzi.
Mzee huyo alikuwa akijiandaa kula chakula cha usiku ndipo aliposikia sauti ya nzi akilia karibu naye aliamua kuchukua kifaa cha umeme kwa ajili ya kuua wadudu ili kufukuza nzi huyo.
Wakati akiendelea na juhudi za kumuua nzi huyo ndipo moto wa kifaa hicho ulipokutana na gesi iliyokuwa ikivuja toka jikoni, moto mkubwa ulilipuka na kuteketeza jiko pamoja na sehemu ya paa la nyumba hiyo. Mzee huyo alijeruhiwa kidogo mkononi.