Hii inakuwa ajali ya kwanza kutokea wiki moja tangu kuzinduliwa kwa majengo ya ghorofa pacha ya One World Trade Centre, New York Marekani.
Watu wawili wanaofanya shughuli za kusafisha vioo vya majengo makubwa na ghorofa, wamepata ajali wakati wakifanya shughuli hiyo katika moja ya ghorofa za One World Trade Centre na muda mfupi baadaye wakaokolewa na Askari wa Kikosi cha Zimamoto.
Kamba za lifti ambayo wanaitumia kufanyia kazi hiyo zilinasa na kugoma kufanya kazi wakiwa ghorofa ya 69, wakajikuta wanakaa bila msaada wowote kwa saa moja na nusu, huku wapita njia walioshtushwa na tukio hilo wakiendelea kuwapiga picha ambazo zimeenea mitandaoni.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook