Chama cha ACT Wazalendo leo walikuwa wakizindua kampeni zao Katika viwanja vya Mbagala Zahkeem kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25.
Pamoja na kuzindua kampeni hizo pia walikuwa wakimtambulisha mgombea wao wa Urais Anna Mghwira kwa wanachama wa chama hicho.
Hapa nimekuwekea maneno ya Kiongozi wa Chama hicho pamoja na Mgombea wao wa Urais
ZITTO KABWE – ‘Kauli mbiu yetu mwaka huu ni utu, uzalendo na Uadilifu, Ni lazima tuzingatie na kuheshimu kauli hii’ #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE- ‘Wenzetu wakisema wanapambana na ufisadi muwaulize wanapambana vipi wakati nchi haina miiko’ #ACT2015 #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE- Ukishakuwa kiongozi wa ACT lazima utangaze mali zako ili tujue umeingiaje na kutokaje madarakani #ACT2015 MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE- Rushwa lazima itaendelea kwenye nchi yetu kutokana na mfumo mbovu wa viongozi waliopo madarakani #ACT2015 #MilardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE- ‘ACT ndio Chama pekee tumesema tutapambana na ufisadi kwa kuheshimu miiko ya Uongozi wa nchi’ #ACT2015 #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-Nchi imekuwa na Mawaziri wakuu 10, NYERERE,KAWAWA,MSUYA,SOKOINE, SALIM,WARIOBA,MALECELA, SUMAYE na PINDA #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-Nchi imekuwa na Mawaziri wakuu 10, NYERERE,KAWAWA,MSUYA,SOKOINE, SALIM,WARIOBA,MALECELA, SUMAYE na PINDA #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE- PINDA na wenzake wanne wanasema wapo na mgombea wa CCM, SUMAYE na LOWASSA wao wapo na UKAWA #ACT2015 #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-Wote wanahubiri mabadiliko,Wanaletaje mabadiliko na watu wale wale ambao waliosababisha shida? #ACT2015 #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-Wenzetu jana wameiba moja ya sera zetu kurudisha Shirika la ndege ACT,walikuwepo wapi siku zote? #ACT2015 MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE- Nawaambia Watanzania hakuna chama kitakacholeta mabadiliko zaidi ya ACT,wengine wanajilazimisha #ACT2015 MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-‘Marais wote waliopita walikuwa wanaume lakini nchi imetamalaki ufisadi, bora tumpe mama tubadilishe gia #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-Wengine wameahidi watatuletea bure elimu ya chekechea hadi chuo kikuu,hatujui watapata wapi Fedha #ACT2015 MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE- Kuna ambao wameahidi kujenga barabara hata sehemu ambazo barabara zipo tayari,hatujui pesa wanapata wapi #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-‘CCM wameahidi kutoa milioni 50 kila kijiji ni sawa na bilioni 600 lakini hawatuambii watazipata #ACT2015 #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-‘Hizo fedha ni sawa na bajeti ya Wizara ya Kilimo, watazipata wapi kama si kuwaongezea ushuru? #ACT2015 #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-‘Mama akija atawaambia mpango wetu kupanua elimu na vyuo vya ufundi, wala msimuulize atazitoa wapi fedha’ #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-Leo hii tunaambiwa ufisadi si ajenda wakati tunaendelea na michakato ya uchaguzi, kuna watu wanapiga hela #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-Kwenye ilani yetu tumesisitiza Uzalendo,namna gani ya kuhakikisha tunajenga mapenzi na Taifa letu #ACT2015 MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-‘Jmosi ijayo Taifa Stars itacheza na Nigeria, tunawaomba TFF watu waingie bure kusherehekea timu yao #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ZITTO KABWE-‘Nani anajua MAGUFULI anashangilia timu gani, mtu wa hivyo akisema anakuza michezo mtamuamini? #ACT2015 #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-Miaka 50 baada ya uhuru Tanzania inahitaji mabadiliko si tu ya kifikra au sera bali na ya kijinsia #ACT2015 #MillardAyoUpadates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-Endapo nitachaguliwa kuwa Rais jambo la kwanza kama mama wa Kitanzania nitatekeleza majukumu muhimu #ACT2015 MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-Mambo makubwa matatu nitakayofanya ni utu,uadilifu na Uzalendo, lazima tulirejeshe Taifa katika misingi bora #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-‘Nitaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, mimi ni mama, mama hukusanya vifaranga vyake pamoja’ #ACT2015 #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-‘Katika kujenga Taifa letu hakuna chama, dini wala itikadi yoyote isipokuwa Taifa moja #ACT2015 #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-‘Katika kujenga Taifa letu hakuna chama, dini wala itikadi yoyote isipokuwa Taifa moja #ACT2015 #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-‘Chama chetu kimeweka na ninaahidi kusimamia vipaumbele vikubwa vinne katika ilani ya uchaguzi #ACT2015 #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-‘Jambo la kwanza ni hifadhi ya Jamii,Watanzania wengi hatuna akiba benki,tunachuma asubuhi na kulala hoi’ #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-‘Mwaka 2016 chini ya Serikali ya Mama tutaweka utaratibu wa kila Mwananchi kujiwekea akiba yake #ACT2015 #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-TZ ina tatizo kubwa la ajira, wengi hatuna uhakika na ajira,tawimu inaonyesha robo tatu wanategemea kilimo #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA -Tafiti zinaonyesha tatizo la ajira nchini na hata nchi nyingine Afrika zinatokana na ukosefu wa maarifa #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-‘ACT chini ya Uongozi wa Mama katika kilimo tutahakikisha kilimo kinatumika kumaliza umaskini #ACT2015 #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA- Ardhi na mashamba yote yaliyokuwepo kwenye Mashirika ya umma tutayarudisha katika uzalishaji #ACT2015 #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-Msukumo utawekwa kwenye bidhaa za nguo kwa sababu zinaajiri watu wengi zaidi na zitapunguza mnyororo #ACT2015 MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-‘Tutakuwa na kazi ya kufufua viwanda kwa sababu vitatusaidia sana kutengeneza ajira kwa Watanzania #ACT2015 #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA- Kuna maeneo mengi nchini ambayo yanaweza kutuletea ajira kama sekta ya Maliasili na Michezo #ACT2015 #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-‘Nchi imejaliwa rasilimali nyingi hasa madini gesi na Mafuta ambavyo havijaonyesha kuwasaidia Watanzania #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-‘Nchi imejaliwa rasilimali nyingi hasa madini gesi na Mafuta ambavyo havijaonyesha kuwasaidia Watanzania #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-Kitila MKUMBO tunamwita Profesa lakini amesoma katika mazingira magumu sana, ningemjua mapema ningemsaidia #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA- ‘Leo tumezalisha watoto wa mitaani na yatima kutokana na mfumo mbovu wa elimu ya Tanzania’ #ACT2015 #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
ANNA MGHWIRA-‘Tanzania ina huduma duni za afya, ni mbovu na ni ghali kupita kiasi,Nafahamu matatizo ya huduma za afya #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) August 30, 2015
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos