Leo Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe pamoja na aliyekuwa mgombea Urais wa chama hicho Anna Mghwira wamezungumza na waandishi wa habari ikiwa ni mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.
Katika mkutano huo Mwenyekiti wa chama hicho Anna Mgwhira alitumia nafasi hiyo kuweza kuwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kuwasuport katika kipindi chote cha kampeni na kukifanya chama kuzidi kuwa imara zaidi.
Zitto Kabwe naye alizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo kumpongeza Mwenyekiri wake Anna Mgwhira kwa kumsaidia kukitangaza chama hicho na kupandisha taswira ya chama chao mbele ya umma.
“Kazi iliyopo mbele yetu ni kukijenga chama na kukifanya kifike mbali zaidi, tumefanikiwa kupata kiti kimoja cha ubunge lakini tutatumia kiti hicho kupaza sauti ndani ya bunge..ikumbukwe sisi tulisema waziwazi kuhusu rushwa tofauti na vyama vingine vya upinzani ambavyo havikuwa wazi”..Zitto
Pia alizungumzia suala ya dawa za kulevya“Nchi nyingi zimeanza kufanya mabadiliko kuhusu dawa za kulevya, dunia nzima imeanza mkakati wa kupambana na dawa za kulevya, ujangili pamoja na rushwa ambayo ndio mambo tutakayokwenda nayo ndani ya bunge ili kuweza kupaza sauti zetu ndani ya jamii inayotuzunguka”..
Pia alimpongeza Rais Dk.Magufuli kwa kuweza kudhibiti safari za nje“Wakati nikiwa Mwenyekiti wa PAC niliagiza kufanywa ukaguzi wa fedha za umma kuhusu safari za nje za viongozi wetu, nataka tu niwahahakikishie Watanzania wenzangu mimi na marehemu Deo FILIKUNJOMBE tuliagiza ukaguzi na upo tayari, wakati wowote tutawaita na kulitolea maelezo ya kina”.
“Kwenda tu katika sehemu na kushtukiza hakutatatua wizi wa mali za umma, tunataka Rais aweke mifumo endelevu ili leo na kesho akiwa hayupo iweze kufanya kazi kwa manufaa ya umma”.
Kuhusu mgogoro wa Zanzibar Zitto amesema “ZEC imefuta uchaguzi lakini ukisoma katiba ya Zanzibar hakuna mahali panaonyesha Mwenyekiti wa Zanzibar ana mamlaka ya kufuta uchaguzi, kama tatizo lilikuwa ni majimbo ya Pemba tume ilipaswa kurudia kuhesabu kura kwenye yale majimbo husika”.
“Mpaka leo tunapozungumza kikatiba Zanzibar haina Serikali, mtu yeyote anayejiita rais wa Zanzibar kikatiba amepindua, anapaswa kushtakiwa kwa kosa la kiuhaini na kosa lake adhabu yake ni kifo, tunamtaka Rais Magufuli ahakikishe tume ya ZEC inatangaza matokeo”.
ANNA MGHWIRA- Niwapongeze watanzania kwa kuonyesha mwelekeo na kuelewa sera na vipaumbele vyetu wakati wa uchaguzi #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ANNA MGHWIRA-Sasa tunajipanga kutaka mabadiliko makubwa ya kikatiba ili rasilimali zetu zimilikiwe na Watanzania wote #MillardAyoLIVEUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ANNA MGHWIRA-Ni wakati wa kuhakikisha tunakiendeleza chama kwa jitihada zote ili kifike mbali kwa masilahi ya WaTZ #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE-Nampongeza mama Anna kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kuzunguka Tanzania nzima na kukitangaza chama chetu #MillardAyoLIVEUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE- Tumefanikiwa kushika nafasi ya tatu kati ya Marais nane waliweza kujitokeza kugombea nafasi ya Urais #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE-Dunia nzima sasa inapambana na madawa ya kulevya, ujangili pamoja na suala la rushwa, tumejipanga #MillardAyoLIVEUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE-Napongeza hatua ya Rais wetu hasa kudhibiti safari za viongozi kuhusu safari za nje, hilo ni jambo kubwa #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE-Kwenda tu katika sehemu kushtukiza hilo halitapunguza tatizo la rushwa, tunaomba aweke mifumo endelevu #MillardAyoLIVEUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE- Kuhusu gharama za viongozi kwenda nje tulianza kulifanyia kazi tukiwa PAC mimi na marehemu FILIKUNJOMBE #MillardAyoLIVEUPADETS
— millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE- Mpaka leo kikatiba Z’bar haina viongozi, na yeyote anayejiita kiongozi kwa sasa ni makosa kikatiba #MillardAyoLIVEUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE-Tunamuomba Rais akae na kuliangalia hili kuhakikisha Z’bar inapata viongozi kikatiba, wananchi waridhike #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE-Rais atumie mamlaka yake waunde Serikali ya mpito, waangalie upya katiba ya Z’bar ili mshindi atangazwe #MillardAyoLIVEUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE-Rais atumie mamlaka yake waunde Serikali ya mpito, waangalie upya katiba ya Z’bar ili mshindi atangazwe #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE- Sio vizuri kuona Rais anaishia tu kwenda Muhimbili huku wenzetu Z’bar bado hawajapata viongozi kikatiba #MillardAyoLIVEUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE- Bunge lijalo nitafanya kazi kwenye kamati yoyote ile ambayo nitakuwa nimepangiwa na Spika #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE-ACT itakuwa tayari kufanya kazi na chama chochote ambacho kitakuwa na ushirikiano kwa manufaa ya wananchi #MillardAyoLIVEUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE- Tatizo la Z’bar si la kikatiba ni la kisiasa, ni lazima limalizwe kisiasa, watu waliamua kufuta matokeo #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
ZITTO KABWE-Wiki inakatika tangu Rais aapishwe, hatujawahi kusikia akizungumzia mambo ya Z’bar, inabidi aingilie kati #MillardAyoLIVEUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 11, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.