Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Saitoti Levilal (42) mkazi kata ya Ilkiding’a wilayani ya Arumeru mkoani Arusha, amedai kuwa amekatwa viganja vya mikono yake na mtu asiyejulikana ikiwa ni baada ya kutaka kumuokoa mwanamke aliyekuwa akiokota kuni asibakwe na mtu huyo katika msitu wa Narok uliopo katika kata hiyo
Saitoti akizungumza na waandishi wa habari akiwa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru), amesema mnamo January 16, 2024 muda wa saa saba kasoro mchana akiwa anachunga ngedere katika mashamba yaliyopo katika eneo hilo, alisikia sauti ya mwanamke ikiomba msaada huku ikitaja jina lake.
Aidha, mjeruhiwa wa pili katika tukio hilo Babu Meijo amesema alikatwa na silaha hiyo aina panga wakati alipoenda kutoa msaada kwa mama huyo