Mshambuliaji wa kimataifa wa Togo aliyekuwa anaichezea klabu ya Tottenham Hotspurs Emmanuel Adebayor alikuwa kimya kwa muda mrefu na kutokueleza chochote kilichomfanya aondolewe katika list ya wachezaji wa Tottenham Hotspurs watakaoshiriki mechi za mashindano mbalimbali. Kuelekea mchezo kati ya Spurs dhidi ya Crystal Palace anayeichezea staa huyo Adebayor amefunga hali ilivyokuwa.
Adebayor aliondolewa kikosini na kukaa bila timu kwa zaidi ya miezi miwili na kuendelea kulipwa mshahara kama mkataba wake unavyoeleza, licha ya kuwa hachezi. Dirisha dogo la January 2016 Adebayor alijiunga na klabu ya Crystal Palace, February 18 Adebayor kaeleza hali ilivyokuwa na wala tatizo halikuwa kwa kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino kama ilivyokuwa bali ni kwa mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs Daniel Levy.
“Kiukweli sikuwa na mahusiano mazuri na mwenyekiti wa klabu Daniel Levy, kwani alifanya mambo yawe magumu, lakini mwisho wa siku nilijua mimi ni nani natoka wapi na una panga kwenda wapi, watu wanaweza kukujaji lakini nilijua mimi nataka nini na nimesimama katika msimamo upi, kiukweli nilikuwa na mahusiano mazuri sana na Mauricio Pochettino ila mwisho wa siku ili bidi aniambie kuwa hawezi kunijumuisha ktika na nilielewa kuwa maisha yangu Spurs yameisha” >>> Adebayor
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE