Emmanuel Adebayor huyu ni staa wa soka kutoka Togo, kwa sasa unaweza muhita ndio staa mwenye jina kubwa kwa wachezaji wanaotokea Togo, mshambuliaji huyo ambaye amewahi kucheza katika klabu ya Arsenal ya Uingereza mwaka 2006 kabla ya mwaka 2009 kuamua kuhamia Man City na mwaka 2011 akajiunga na Tottenham Hotspurs ambayo imemuondoa kikosini.
Licha ya kuwa Adebayor kwa sasa yupo nje ya uwanja kwa muda wa miezi kadhaa, baada ya kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino kumuondoa katika list ya wachezaji wake ambao atawatumia katika michuano ya Ligi Kuu Uingereza na michuano ya Europa League, staa huyo yupo nje ya uwanja toka mwezi September 2015.
Hata kama Emmanuel Adebayor hayupo katika klabu ya Tottenham kwa sasa, klabu hiyo inalazimika kumlipa Adebayor mshahara wa pound 100,000 kwa wiki kama kawaida, ambazo ni zaidi ya milioni 300 za kibongo kwa wiki, kama Adebayor hatopata timu hadi mwezi June mwakani.
Spurs watamlipa staa huyo pound milioni 5 ambazo ni zaidi ya bilioni 15 za kibongo.Staa huyo kwa sasa yupo kwao Togo ila anaripotiwa kuwa na mipango ya kwenda London kufanya mipango ya kujiunga na klabu nyingine za jiji hilo katika dirisha dogo la usajili la mwezi January 2016.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.