Wimbo wa Adele umekuwa wimbo mkubwa sana, wimbo ambao huenda ukawa mmoja kati ya ngoma ambazo zimerudiwa kwa kuimbwa cover yake na watu wengi zaidi duniani… lakini unajua kwamba rekodi zinaonesha wimbo huo una kama siku 88 tu hewani, hesabu ambayo kwa tafsiri nyingine ni miezi mitatu !!
Ninayo stori ambayo wameiandika pia kwenye page ya CNN mtandaoni kwamba wimbo wa ‘Hello‘ uliomrudisha Adele kwenye kilele cha kusikilizwa kwa mara nyingine, wimbo huo umetazamwa mara bilioni 1 kwenye channel ya Youtube.
Ngoma hiyo inakuwa ya 17 kuingia kwenye rekodi ya kutazamwa na watu zaidi ya bilioni 1 kwenye mtandao huo.
Rekodi zinaonesha mwaka 2013 wimbo wa ‘Roar‘ staa wa Marekani, Katty Perry uliingia kwenye rekodi ya kutazamwa mara bilioni moja baada ya siku 487, mwaka 2014 kukawa na rekodi ya wimbo ‘Black Space‘ wa Taylor Swift uliingia rekodi ya kuangaliwa mara bilioni moja baada ya siku 238.
Mwaka 2015 umekuwa mwaka wa Adele, wimbo ‘Hello‘ umeingia kwenye rekodi hiyo ndani ya siku 87, huenda ndio wimbo ambao umetazamwa na watu wengi zaidi ndani ya siku chache kwenye rekodi za Youtube.
Adele huyu hapa na ‘Hello‘ yake mtu wangu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE