Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji NIT Zakaria Mganilwa ameeleza kuwa chuo kimepokea taarifa rasmi ya kifo cha mwanafunzi Aquilina Akwilini aliyepigwa risasi na kufariki jana February 16, 2018 wakati polisi wakizuia maandamano ya wafuasi wa CHADEMA katika eneo la Mkwajuni.
Ameeleza Chuo kiliwatuma mwakilishi wa Bodi ya Usimamizi wa chuo, Mwangalizi wa Wanafunzi, pamoja na mwakilishi mwingine wa Serikali ya Wanafunzi katika chuo hicho kwenda kutambua mwili wa marehemu katika Hospitali ya Mwananyamala.
Tayari wamekwishafanya mawasiliano na familia ya marehemu ambao wanaishi Mbezi ya Kimara, na mpaka sasa wawakilishi hao wametumwa kwenda kuonana na familia.
“Gari la Washawasha lipo na ikifika Muda litatumika” – Kamanda Kilimanjaro