Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF August 18 kupitia kwa afisa habari wa shirikisho hilo Baraka Kizuguto limethibitisha kumkosa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza katika klabu ya Mansfield Town inayoshiriki Ligi daraja la tatu Uingereza Adi Yussuf.
TFF imethibitisha kumkosa mshambuliaji huyo kwa sababu amepata majeruhi hivi karibuni hivyo klabu yake ya Mansfield Town imeomba kutojumuishwa kwa mshambuliaji huyo katika kikosi cha Taifa Stars kitakachosafiri August 22 kuelekea Oman kwa ajili ya mechi ya kirafiki kabla ya kwenda kuweka kambi Instabul Uturuki kwa kambi ya maandalizi zaidi ya mechi ya kufuzu AFCON 2017 dhidi ya Nigeria.
Adi Yussuf ambaye alitangazwa kuitwa katika kikosi cha Taifa Stars alizaliwa February 20 1992 visiwani Zanzibar lakini amewahi kucheza katika klabu ya Leicester City. Sambamba na hayo TFF imetangaza kufungwa kwa dirisha la usajili siku ya Alhamisi ya August 20 na timu itakayoshindwa kumaliza usajili ndani ya muda huo italazimika kulipa Tsh laki 5.
“palikuwa na mshambuliaji Adi Yussuf ambaye anacheza Mansfield Town ya Ligi daraja la tatu nchini Uingereza mwalimu alimuita kwa ajili ya kujiunga na kikosi chake, taratibu zilifanyika za mchezaji huyu na alikuwa aungane na timu itakapokuwa kambini nchini Uturuki lakini katika mchezo aliocheza mwishoni mwa wiki alipata majeruhi”>>>Kizuguto
Msikilize Kizuguto akikupa ratiba ya Stars
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos