Mchekeshaji na balozi wa Asas Mwalubadu amesafiri kutokea Norway hadi Cairo Misri kwa ajili ya kuishangailia timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, inayoshuka dimbani leo kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Senegal katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi.
Mwalubadu ambaye amezoeleka kwa vichekesho na kujiita yeye ndio mwenyekiti wa kamati ya roho mbaya ya Taifa Stars, ametania kuwa amekuja na waganga kutokea Songea Tanzania hivyo haoni namna kwa nguvu yake na swahiba wake Manara wanaweza kuisapoti Tanzania na ikashinda.
EXLUSIVE: EMMANUEL OKWI BAADA YA KUKABIDHIWA TUZO AFCON 2019